Select your language

Historia - Usuli

Shirika la Maendeleo la Ujerumani, kupitia Shirika lake la Msaada wa Kiufundi na Mikopo ni, moja ya washirika wa maendeleo wa kawaida wa serikali ya Tanzania katika sekta ya maji.

Katika miaka iliyopita, mafanikio makubwa yamepatikana katika sekta ya maji ya Tanzania. Chini ya Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP Awamu ya I, kuanzia 2007 hadi 2014) takribani watu milioni 4.2 vijijini na watu milioni 2.8 mijini wameweza kupata maji ya kunywa.

Hata hivyo, katika mwaka 2015 ni 77% tu ya wakazi wa mijini na 56% ya wakazi wa vijijini waliweza kupata huduma ya maji ya kunywa kutoka vyanzo vilivyoboreshwa (WHO na UNICEF: Maendeleo kuhusu usafi na maji ya kunywa  - mrejesho wa 2015 na tathmini ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia “MDG”). Kwa hiyo, ili kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu (upatikanaji wa huduma za maji safi na maji taka kwa wote ifikapo 2030) itakuwa ni changamoto.

Licha ya uzoefu kutoka awamu ya I ya WSDP imeonesha pengo dhahiri la viwango vya huduma za umma katika maeneo ya mijini. Pengo hili linatokana na ongezeko la haraka la idadi ya watu katika maeneo ya mijini kutokana na ukuaji wa miji, ambao hauendani na uwekezaji mdogo katika miundombinu ya maji. Ukweli kwamba, miradi mingi iliyotekelezwa katika Awamu ya I ilihusisha kuongeza uzalishaji wa maji bila ya kuzingatia mfumo wa usambazaji wa maji, ilikuwa changamoto nyingine kwa sababu mitandao mingi ya uzalishaji na usambazaji maji katika mikoa na wilaya za mijini ni chakavu na inahitaji ukarabati.

Ili kurekebisha hali hiyo, vyanzo vipya vya fedha kama vile mikopo ya kibiashara inahitajika. Vile-vile inabidi kuharakisha utekelezaji, ambao unahitaji kuimarisha na kuongeza uwezo wa kuji-tegemea katika utoaji wa huduma za umma katika usambazaji wa maji safi na uondoshaji wa maji taka mijini (Mamlaka za Maji Safi na Maji Taka Mijini).

Hii ndiyo maana Wizara ya Maji (MoW) na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) mwaka 2014 zilikubaliana kuanzisha Mikopo ya Uwekezaji kwa ajili ya Mamlaka za Maji Safi na Maji Taka Mijini (UWSSAs). Mikopo hiyo ya Uwekezaji (IFF) imezisaidia Mamlaka za Maji Safi na Maji Taka Mijini nchini Tanzania kugharimia uwekezaji wa miundombinu yenye kuweza kuzalisha mapato kwa haraka (yaani; uunganishaji wa huduma ya maji katika maeneo mapya, ubadilishaji wa mabomba chakavu au ufungaji wa mita za maji) kwa kutumia mikopo ya kibiashara kutoka benki za ndani.

Mikopo hiyo ya Uwekezaji (IFF) ni msaada unaozingatia matokeo, ambapo Mamlaka za Maji Safi na Maji Taka Mijini (UWSSA) zitapatiwa malipo ya bonasi kutokana na “dirisha la Mkopo wa Uwekezaji/Msaada unaotegema Matokeo” mara malengo ya wakati uliopita ya utekelezaji yata-kapokuwa yamefikiwa. Malipo haya ya bonasi yanachukua hadi 50% ya jumla ya gharama zote stahiki za uwekezaji kwa mradi husika kama msaada kiasi kisichozidi Euro milioni moja. Motisha hii inaweza kutumika kurejesha mkopo na/ au kugharimia uwekezaji mwingine unaohitajika ili kuongeza kiwango cha huduma au kuongeza wigo wa usambazaji wa Maji safi na uondoshaji wa Maji taka.
Kuanzia mwaka 2014 hadi mwaka 2016, kampuni ya MACS Energy and Water (MACS) ilipewa mkataba kwa ajili ya awamu ya majaribio ya Mikopo ya Uwekezaji (IFF).
Tangu mwezi Aprili 2016, kampuni ya GFA Consulting Group GmbH, kwa ushirikiano na JBG Gauff Consultants pamoja na NETWAS Tanzania, zimekuwa zikitoa huduma za ushauri kwa ajili ya kuwezesha utekelezaji wa utoaji wa Mikopo ya Uwekezaji na Misaada ya Utekelezaji (IFF-OBA) kwa ajili ya Huduma ya Usambazaji wa Maji Mijini, kama muendelezo wa shughuli za ma-jaribio. Muda wa mkataba ni miezi 42 (miaka 3.5). Mshauri anasaidia katika utekelezaji wa mradi kwa kuzingatia mambo matatu:

  • Kuzisaidia Mamlaka za Maji Safi na Maji Taka Mijini (UWSSA) katika uandaaji wa map-endekezo ya kutosha ya miradi ya uwekezaji na maombi ya mikopo ya kibiashara.
  • Kuisaidia Wizara ya Maji katika kuongoza, kuelekeza na kusimamia programu ya Mikopo ya Uwekezaji na Misaada ya Utekelezaji (IFF-OBA). Hii pia inajumuisha kuisaidia Wizara ya Maji (MoW) katika kutimiza matakwa ya kutoa ripoti.
  • Kuzishawishi benki zinazoshiriki katika kujenga uwezo wa ndani wa kuanzisha bidhaa ya mikopo inayolenga Mamlaka za Maji Safi na Maji Taka Mijini (UWSSA) na kusimamia mikopo ya miundombinu.