Select your language

Wabia

Mkopo wa Uwekezaji na Msaada wa Utekelezaji (IFF – OBA) ilianzishwa na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) pamoja na Wizara ya Maji na Umwagiliaji (MoWI). Mradi wa Mikopo ya Uwekezaji unaendeshwa chini ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia Kurugenzi ya Usambazaji Maji Mijini.
Kampuni ya GFA Consulting Group GmbH kwa ushirikiano na JBG Gauff Consultants na NETWAS Tanzania zinaisaidia Wizara ya Maji na Umwagiliaji (MoWI) ambayo ndiye Wakala Mkuu wa Utekelezaji wa Mradi katika masuala yote ya utekelezaji waProgramu ya Mikopo ya Uwekelezaji na Misaada ya Utekelezaji.
Mradi wa Mikopo ya Uwekezaji na Misaada ya Utekelezaji (IFF– OBA) ulianzisha Kamati ya Utekelezaji ambayo inasimamia uendeshaji wa programu. Kamati hii imeundwa na wajumbe kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji (MoWI) na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW), pamoja na wajumbe kutoka Wizara ya Fedha (MoF) na mdhibiti, ambaye ni EWURA.
Kama walengwa wa mradi, Mamlaka za Maji Safi na Maji Taka na benki za biashara pia ni wadau muhimu.
Washirika wengine muhimu ndani ya sekta ya maji ya Tanzania ni GIZ, Benki ya Dunia na Chama cha Watanzania Wasambazaji Maji (ATAWAS).